Published On: Tue, Apr 25th, 2017

Dunia yaadhimisha siku ya Malaria

Share This
Tags

 

Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya Malaria shirika la afya duniani WHO limefahamisha kuwa chanjo ya kwanza ya ugonjwa huo itaanza kufanyiwa majaribio nchini Kenya, Malawi na Ghana kuanzia mwaka 2018.

Chanjo hiyo iitwayo RTS,S ni kwa ajili ya kuwakinga watoto wadogo dhidi ya aina mbaya ya malaria inayosababishwa na mbu aitwae Plasmodium falciparum.

Haijathibitika kwamba chanjo hiyo inaweza kufanya kazi kwa asilimia mia moja, lakini wataalamu wa masuala ya afya wanasema chanjo hiyo ni hatua muhimu katika mapambano ya dunia dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Ripoti ya WHO kwa miaka miwili mfululizo 2015-2016 imebaini kwamba zaidi ya asilimia arobaini ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa malaria na pia kwa mujibu wa ripoti hiyo DRC na Nigeria zimekuwa nchi za kwanza duniani kuathiriwa na ugonjwa wa Malaria.

WHO inasema Kenya Ghana na Malawi ndizo nchi zilizochaguliwa kwa uchunguzi huo kutokana na kuwa nchi zote hizo zina mipango thabiti ya kinga lakini bado zina visa vingi vya malaria.

 

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>