Published On: Tue, Mar 21st, 2017
Business | Post by jerome

WASIOONA NA KUSIKIA WAPEWA ELIMU YA UTAMBUZI FEDHA BANDIA.

Share This
Tags

Watu wenye ulemavu wakiwemo wasioona, wasiosikia wamepewa
mafunzo ya kutambua noti halali na bandia kwa lengo la kuwaepusha kutapeliwa katika shughuli zao.

Mafunzo hayo ya siku moja,yametolewa na watumishi wa Benki Kuu
Tanzania,Mjini Tabora ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo kwa wananchi na
watu walio katika makundi maalum.

TATU HALFANI,ABDALAH MGALULA na SALUMU ALLY, ni miongoni mwa walemavu
waliopata mafunzo hayo wameishukuru BENKI na kusema awali walikuwa
hawatambui noti bandia ikoje na kupelekea kuibiwa na kutapeliwa.
PATRICKY  FATAH ni mmoja wa wakufunzi kutoka makao makuu ya Benki kuu
Dar es salaam, amesema njia kuu za kugundua noti bandia ziko nne
ikiwemo kuangalia sura ya Baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage
Nyerere.

VICKY MSINA ni Meneja msaidizi idara ya uhusiano wa uma beki kuu ya
Tanzania, amesema lengo la kutoa elimu hiyo
kwa makundi maalumu ni kuwawezesha kutambua alama zilizopo kwenye noti
sahihi na kuzitunza ili ziweze kudumu kwa muda mlefu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>