Published On: Tue, Mar 21st, 2017
Business | Post by jerome

WAKULIMA TANGA WALIZWA NA MDUDU “KANTANGAZE”.

Share This
Tags

MDUDU Kantangaze amevamia mashamba ya wakulima na kuharibu vibaya mazao ya matunda na mbogamboga katika kata ya Lukozi wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Mdudu huyo ambaye huharibu mazao ya mimea ameenea katika maeneo mbalimbali na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima wa wilaya ya Lushoto.


Ofisa kilimo  kata ya Lukozi Abasi Mohamed ,amesema mdudu huyo amewaathiri wakulima kwa kiasi kikubwa.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Lucus Shemndolwa amesema ipo haja ya wataalamu wa kilimo kukutana kuona namna ya kupambana na mdudu huyo.

Dawa ya kupambana mdudud huyo inapatikana lakini inauzwa kwa bei ya juu wakulima kushindwa kukabiliana na mdududu huyo.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ametembelea wakulima hao katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo,kuzungumza na wananchi, viongozi wa vijiji na kata.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>