Published On: Tue, Mar 7th, 2017
Business | Post by jerome

VIROBA VYAUZWA KWA SIRI.

Share This
Tags

Licha ya tamko la Serikali la kuanza kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara wanaoendelea kufanya biashara ya pombe zilizo katika vifungashio maarufu kama viroba, imebainika kuwa bado idadi kubwa ya wafanya biashara wa pombe hizo wanaendelea kukaidi agizo la Serikali.

Timu za wakaguzi zinazoendelea kufanya msako katika maeneo mbali mbali jijini Dar es Salaam, na kufanikiwa kukamata shehena ya pombe hiyo ambayo ni katoni zaidi ya elfu 24 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi billion tatu.

Afisa kutoka mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA JOHN NZILA amesema mzigo huo umepatikana maeneo ya kimara temboni, jijini humo.

Nae mwanasheria wa baraza la usimamizi wa mazingiranchini NEMC MACHARI HECHE, licha ya kuwataka wananchi kushiriki katika kutokomeza pombe hiyo, lakini pia hali waliyoikuta kwa wafanyabiashara wa Tegeta ambao wanauza pombe hizo.

Kuendelea kwa  misako hiyo kunatokana na agizo la Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA kutaka pombe ya viroba ikomeshe kote nchini .

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>