Published On: Tue, Mar 14th, 2017
Business | Post by jerome

UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI

Share This
Tags

Licha ya Tanzania kuwa Nchi ya Tatu Barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya Mifugo, bado sekta ya Maziwa haijaweza kutoa mchango mkubwa katika kuchangia pato la Taifa huku mwamko wa wananchi katika unywaji wa Maziwa ukiwa Duni.

Naibu waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi WLLIAM OLE NASHA ameeleza kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha inahimiza unywaji wa maziwa na uzalishaji ilikuhakikisha sekta hiyo inachangia ukuaji wa uchumi.

Waziri OLENASHA amebainisha hayo wakati wa mkutano uliokutanisha wadau wa maendeleo zikiwemo taasisi za kifedha na wazalishaji wa maziwa unaolenga kuinua sekta hiyo.

Baadhi ya wazalishaji wa maziwa akiwemo Meneja kiwanda cha Tanga Fresh MICHAEL KARATA na Meneja mipango kiwanda cha ASASI wakaeleza mkakati wa kuhamasisha unywaji wa maziwa.

Tayari Serikali imeandaa kampeni ya “Okoa jahazi,Jenga Afya, Jenga uchumi kupitia Maziwa” inayolenga kuleta mapinduzi katika sekta ya maziwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>