Published On: Tue, Mar 21st, 2017
Business | Post by jerome

SIDO YAWAPIGA TAFU WAKULIMA WA MIHOGO PWANI.

Share This
Tags

SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogovidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani katika kuunga kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kupambana na wimbi la umasikini limevisaidia kuvikopesha vikundi viwili  vya ujasiriamali  kiasi cha shilingi milioni tatu kwa ajili ya kuweza kuwasaidia kujiendeshea katika shughuli zao za kilimo kwa kuweza kuzalisha na kusindika wenyewe zao la muhogo

Akizungumza na baadhi ya viongozi na wajumbe wa vikundi  hivyo vya ujasiriamali vya Tuwenao pamoja  Mponga   vilivyopo Wilayani Mkuranga  katika halfa fupi iliyofanyika katika kiwanda kidogo cha kusindikia muhogo Meneja wa SIDO Mkoa wa Pwani  Agness Yesaya amesema kuwa wameamuakuvisaidia vikundi  vya wajasiliamari wadogo waliopo vijijini kwa lengo la kuweza  kuwawezesha ili kuwainua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

Meneja Yesaya  amesema kwamba wamebaini katika maeneo mengi ya vijiji kuna fursa nyingi zilizopo katika zao la muhogo lakini wamebaini kuwepo kwa baadhi ya wajasiriamali wanshindwa kutimiza malengo yao waliyojiwekea kutokana na kukosa mtaji wa fedha hivyo wakiwezeshwa wataweza kutumia fursa zilizopo za kilomo kwenye   maeneo yao ili kuleta mabadiliko chanya ya kukuza uchumi.

Kwa  upande wake Mwenyekiti wa Kikundi cha ujasiliamari cha  Tuwenao kilichopo katika kijiji cha Visegese Sophia Mwaya amelipongeza shirika la Sido kwa kuwapatia mkopo huo licha ya kukabiliwa na changamoto ya sugu ya kuharibiwa mazao yao  mashambani na wanyama pori ikiwemo na ugonjwa wa bato bato hivyo  kuiomba serikali kuliingilia kati suala hilo kwani linawarudisha nyuma kimaendeleo na kujikuta wanakosa chakula.

 

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>