Published On: Fri, Mar 10th, 2017

Mwananyamala hospitali kupima Saratani ya Tezi Dume

Share This
Tags

Na Austin Beyard.

Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani huku ugonjwa huo  ukiwa ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.

Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25.

maneno ya vijiweni mara nyingi huleta upotoshaji katika mambo ya msingi ya kijamii na huaminiwa na watu wengi kuwa lisemwalo lipo na hata kama halipo linakuja.

Ugonjwa wa saratani ya tezi dume pia umekumbwa na matatizo ya maneno ya mtaani kuhusu namna madaktari wanavyopima ugonjwa huo huku wengi wakihusisha madaktari kutumia kidole katika upimaji huo.

Dkt ISIDORE KIWALE ni Daktari Bingwa wa upasuaji katika hospitali ya mwananyamala ambaye anaeleza namna wanavyopima saratani ya tezi dume.

Akizungumzia dalili za TEZI DUME, dakta THADEO MAINA  amesema dalili za tezi dume ni pamoja na mtu kuenda haja ndogo mara kwa mara au kupata maambukizi ya U.T.I kila wakati.

Katika kuwawezesha wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam na viunga vyake kupima magonjwa mbali mbali yakuambukiza na yasiyoambukiza hospitali ya mwananyamala ameanzisha kampeni ya upimaji bure kwa siku za wikiend kuanzia jumaa hili hadi jumaa lijalo huku kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo akiwataka wanawake kuwasihi wenza wao kujitokeza kwenye kampeni hiyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>