Published On: Fri, Mar 3rd, 2017
Business | Post by jerome

HARAKISHENI MCHAKATO WA KURIDHIA MKATABA WA KUPUNGUZA MATUMIZI YA ZEBAKI

Share This
Tags

NA JAMES LYATUU

 

Tanzania imeshauriwa kuharakisha Mchakato wa kuridhia mkataba wa Minamata wa kupunguza matumizi ya Zebaki kwenye machimbo madogo ya dhahabu kutokana na kemikali hiyo kuhatarisha maisha ya wananchi wanaozunguka migodi.

Hatua hiyo imekuja baada ya utafiti mpya uliofanyika kubaini uchafuzi wa mazingira utokanao na Zebaki katika machimbo madogo ya dhahabu ambapo imekuwa ikisababisha serikali kupoteza mabilioni ya fedha kutokana na kemikali hiyo.

Akizungumza kuhusiana na utafiti huo, Afisa Mwandamizi taasisi ya AGENDA inayojihusisha na usimamizi wa mazingira HAJI REHANI ameeleza kuwa utafiti huo ulihusisha sampuli za nywele kwa wananchi wanaozungukwa na machimbo.

Kwa upande wake Afisa Programu mkuu wa shirika hilo SILVANI MNG’ANYA ameeleza kuwa serikali inapaswa kuchukuwa hatua za haraka kabla kuongezeka kwa athari.

Utafiti huo ulipama viwango vya zebaki katika nywele za watu 236 kutoka nchi 15 ikiwemo Tanzania, Kenya, Cameroon, India Uruguay na Indonesia.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>