Published On: Wed, Mar 15th, 2017
Business | Post by jerome

GHARAMA ZA KUKOPA SASA KUPUNGUA

Share This
Tags

Hivi karibuni benki kuu ya Tanzania imepunguza riba (Discount Rate) kwa benki zinazohitaji ukwasi kupitia dirisha la benki kuu la discount ambapo benki hizo zitaweza kukopa kwa gharama nafuu zaidi.

Kuanzia mwezi Julai 2016 hadi Februari 2017, kasi ya ongezeko la ukwasi kwenye benki za biashara imekuwa ikipungua, hali hii ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na kupungua kwa fedha za kibajeti kutoka nje ya nchi ikiwemo fedha za wahisani na mikopo ya kibiashara.

Katika jitihada za kuongeza ukwasi, Benki Kuu imefanya tathmini ya mwenendo wa riba katika soko la dhamana za serikali, mfumuko wa bei nae maeneyo mengine na kulazimika kufanya mapitio ya riba upya.

PETER MAKAU ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benk ya United Bank of Africa (UBA) ambaye amebainisha kuwa hatua hiyo itawawezesha benki za kibishara kukua.

Makau amesema hatua hii itaziwezesha benki za biashara nchini kukabiliana na tatizo la ukwasi katika sekta ya fedha nchini kwani benki nyingi zitakuwa na uwezo wakokopa na kuwakopesha wananchi kwa bei nafuu.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashine maalum za kutolea fedha za benki ya UBA mwenyekiti wa bodi ya UBA Generali mstaafu Robert Mboma amesema ni muhimu kwa watanzania kujiwekea akiba.

Mapema mwezi huu, Benki kuu ya Tanzania imepunguza riba (discount rate) kutoka asilimia 16.0 iliyotumika tangu mwezi Novemba 2013, hadi asilimia 12.0 ambayo imeanza kutumika rasmi tarehe 6 Machi 2017.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>