Published On: Tue, Mar 21st, 2017

BUIBUI ATAJWA KUWA TIBA YA KIHARUSI.

Share This
Tags

Protini katika sumu ya buibui inaweza kusaidia kulinda ubongo kutokana na jeraha baada ya kiharusi kulingana na utafiti.

Wanasanyasi waligundua kwamba tiba ya protini Hi1a ilifanya kazi ilipotumiwa katika panya wa maabara.

Wanasema kuwa ilionyesha kwamba inaweza kuwa tiba nzuri katika siku za usoni ya kiharusi lakini haijajaribiwa miongoni mwa binadamu.

Muungano unaopigana dhidi ya ugonjwa wa kiharusi umesema kuwa utafiti huo bado ungali katika awamu ya kwanza lakini unaunga mkono tiba yoyote inayoweza kupunguza uharibifu unaofanywa na kiharusi.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Queensland and Monash , walisafiri hadi kisiwa cha Fraser nchini Australia kuwawinda na kuwasika buibui hatari wa taifa hilo.

Baadaye waliwachukua buibui hao katika maabara ili kuwatoa sumu hiyo.

Hatua hiyo ilishirikisha kuwabembeleza buibui hao kutoa sumu hiyo ambayo baadaye hutolea kwa kupitia bomba.

Walitoa protini hiyo na kutengeza kadhaa katika maabara.

Baadaye walimdunga panya protini hiyo ambapo iliweza kuzuia jeraha lolote katika ubongo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>