Published On: Tue, Mar 14th, 2017
Business | Post by jerome

B.O.T KUWEKA SHERIA YA UTUNZAJI FEDHA

Share This
Tags

BENKI kuu ya Tanzania imesema kuwa imeanza kuandaa mchakato wa kuifanya serikali kutunga sheria kali itakayolazimisha watu mbalimbali kuwa na utaratibu maalum wa kutunza pesa ili zisiharibike kwa haraka.

Afisa Mwandamizi wa Benki kuu ya Tanzania,Patrick Fata amesema hayo katika mafunzo ya siku moja ya utambuzi wa fedha bandia kwa watu wenye ulemavu wa kusikia kutoka kikundi cha sanaa na utamaduni kwa viziwi Tanzania (KISUVITA).

Fata amesema kuwa mpango huo wa benki kuu unakuja kufuatia baadhi ya watu kutofuata taratibu na matumizi sahihi ya utunzaji wa fedha hivyo kufanya fedha nyingi kuharibika katika kipindi kifupi na kwamba kuwepo kwa sheria kutawalazimisha watu mbalimbali kufuata sheria hiyo ikiwemo kuwalazimisha kutunza fedha zao kwenye pochi.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi idara ya uhusiano wa umma,Vicky Msina amesema kuwa mkoa Kigoma ni moja ya mikoa ambayo inakabiliwa na utunzaji hafifu wa fedha na hivyo sehemu kubwa ya pesa za Tanzania kuharibika kwa muda mfupi na hivyo elimu ya utunzaji sahihi wa pesa inahitajika kiasi kikubwa.

 

Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa wilaya Kigoma,Samon Anga ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma,Emanuel Maganga amekiri kuwepo kwa tatizo la utunzaji hafifu wa fedha mkoani humo na kwamba serikali itaendelea kutoa elimu kuhusiana na matunzo sahihi ya fedha lakini kuchukua sheria kwa watu wanaoharibu fedha hizo kwa makusudi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>