Published On: Mon, Mar 6th, 2017

ADELE ATANGAZA KUOLEWA!

Share This
Tags

Msanii wa muziki Adele amethibitisha kwamba ameolewa na Simon Konecki baada ya miezi kadhaa ya uvumi.

Mwanamuziki huyo alikuwa jukwaani huko mjini Brisbane Australia akizungumza kuhusu wimbo wake Someone Like You ,wakati aliposema ,”nimeolewa sasa”.

Kumekuwa na uvumi kwamba wawili hao walioana na kwamba Adele alimtaja kuwa mumewe katika tuzo za Grammy.

Adele na Simon wana mtoto mmoja pamoja-mvulana wa miaka 4 anayejulikana kama Angelo.

Kanda ya video inayomuonesha Adele akizungumza kuhusu ndoa yake imesambazwa katika mitandao ya kijamii.

Alikuwa akielezea wakati alipoimba wimbo ”Someone Like You” kwa familia yake na marafiki aliposema kwamba ”ameolewa”.

”Niliona katika macho yao wakati walipokuwa wakisikiza kwamba ilikuwa ikiwakumbusha kuhusu kitu ama mtu”.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>