Published On: Fri, Feb 17th, 2017

WAHUDUMU WA AFYA WANAOWANYANYASA WENYE KADI ZA NHIF KUKIONA

Share This
Tags

Vituo vya afya, zahanati  pamoja na hospitali ya rufaa ya mkoa wa mara zimetakiwa kuboresha huduma za  matibabu za mfuko wa bima ya afya ili kuendana na malengo ya mfuko huko katika kuwahudumia wananchi.

Wakiongea katika mkutano kati ya wadau na wahudumu wa mfuko wa bima ya afya uliofanyika mjini Musoma mkoani Mara baadhi ya wanachama wa mfuko huo wamesema wanakutana na changamoto nyingi kwa watoa huduma za afya kupitia mfuko huo.

Wamesema mbali na kutoa malalamiko juu ya huduma mbaya wanazopata lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.

Musa Marwa ni moja wa wananchama wa mfuko huo waliohudhuria katika kikao hicho ameitaka serikali kuwachukulia hatua watumishi wote wanaokwenda kinyume na malengo ya mfuko huo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa ameeleza kutoridhishwa na utoaji huduma za mfuko huo na kuzitaka Halimashauri zote za mkoa Hhuo pamoja na hospitali ya mkoa kuboresha huduma za mfuko wa Bima ya Afya.

Kutokana na kuwepo na malalamiko mengi toka kwa wanachama wa mfuko huo mwenyekiti wa bodi ya NHIF Anne Makinda ametumia mkutano huo kueleza hatua zitakazo chukuliwa kwa wahudumu wa mfuko wa bima ya afya atakaekwenda kinyume na malengo ya mfuko huo.

Amesema wahudumu wanaowanyanyasa wateja au wanachama wa NHIF pindi wanapokwenda kutibiwa wanapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kuwa lengo la mfuko huo ni kutoa huduma bora kwa wananchi.

= = = = =

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>