Published On: Thu, Feb 16th, 2017

UTAPIAMLO WAWAKABILI WATOTO NCHINI

Share This
Tags

NA RACHEL CHIZOZA

 

 

Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye Utapiamlo Afrika licha ya kushuka kwa idadi ya watoto wenye tatizo hilo nchini kutoka asilimia 42 mwaka 2010 na kufikia asilimia 34 mwaka 2015.

Licha ya elimu ya Lishe kutolewa mara kwa mara bado tatizo la utapiamlo linawakabili watoto nchini, wengi wao wakiwa wale wanaoishi vijijini.

Takwimu hizo zikaifikisha Clouds kwenye Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam na kuzungumza na Daktari Kiongozi wa hospitali hiyo OMARY MAHIZA ambaye amekili uwepo wa tatizo hilo

Mmoja wa wazazi wa watoto waliolazwa kwenye Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam amesema wamekuwa wakifundishwa namna ya kuondokana na tatizo hilo.

Pamoja na watoto kuathiriwa na mfumo wa ulaji usiofaa wanawake pia huathirika kwa kupungukiwa damu.

Tiba ya Utapiamlo ni kula mlo kamili.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>