Published On: Thu, Feb 16th, 2017

MPINA AKITOZA FAINI YA SHILINGI MILIONI 25 KIWANDA CHA CHEMICOTEX

Share This
Tags

Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amekitoza faini ya shilingi Milioni 25, kiwanda kinachotengeneza biadhaa mbali mbali za matumizi ya manyumbani kama vile mafuta ya kujipaka mwili na dawa za meno cha chemicotex, mkilichopo Mbeji Jogoo jijini Dar es Salaam Kwa uchafuzi wa mazingira.

Faini hiyo inayotakiwa kulipwa baada ya wiki mbili inatokana na ukiukwaji mkubwa wa sheria ya mazingira unaofanywa na kiwanda hicho kilichopo katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi, ya kutiririsha maji taka na maji machafu katika mfereji wa maji ya mvua.

Naibu Waziri Mpina ameshangazwa na uthubutu wa uchafuzi wa mazingira unaofanywa na kiwanda hicho, pamoja na jitihada za serikali kupitia Ofisi yake na NEMC za kuthibiti uharibifu wa mazingira kwa kutoa adhabu mbali mbali kwa waharibifu.

“Ujio wangu katika kiwanda hiki unatokana na malalamiko ya wananchi ya kututiririshiwa maji machafu katika makazi yao na maeneo ya biashara, hakuna atakaesalimika kwa kosa la kutokutunza mazingira na afya za watu, alisistiza Mpina”.

“Mpo Barabarani mnachafua mazingira Hadharani bila haibu, mmedharau jitihada za serikali hii ya awamu ya tano na kuona kama ni nguvu za soda, adhabu hii ilipwe kama ilivyo elekezwa hatuta kuwa na uvumilivu kwa muwekezaji yeyote atakaechafua mazingira. Alisema”.

Kwa Upande wake Mwanasheria kutoka NEMC Bw. Heche Mananche aliongeza kwa kusema kuwa Mmiliki wa kiwanda endapo hatakuwa tayari kulipa faini hiyo anaweza kupelekwa mahakamani.

Wakati Huo Huo, Naibu Waziri Mpina Amezindua Mfereji wa kutirirsha maji katika kiwanda cha Cement cha wazo, baada ya kujiridhirisha na utekelezaji wa maagizo yake kiwandani hapo katika moja ya ziara zake

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>