Published On: Fri, Feb 24th, 2017

AMBER LULU “SIPIGI PICHA KUJIUZA MITANDAONI, NAPIGA KWA MAPENZI YANGU”

Share This
Tags

Video Queen anaetamba katika ngoma za wasanii mbalimbali nchini Lulu Auggen Maarufu kama ‘Amber Lulu’ amesema kuwa hapigi picha za utupu kwa lengo la kujiuza mtandaoni na badala yake amekuwa akipiga picha hizo kwa mapenzi yake.

Amber Lulu ameeleza hayo katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Runinga ya Clouds Tv ambapo amewaonya wale wanaomuiga kwa kupiga picha za Utupu.

“Nashangaa baadhi ya watu wanaoniiga kupiga picha hizi, mimi sipigi hizi picha ili watu waniige bali napiga picha hizi kama starehe yangu sasa hao wanaoniiga sioni kama ni sahihi” Alisema Amber Lulu.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>