Published On: Tue, Jan 10th, 2017

wizara ya afya yaeleza ulevi unavyoweza kuathiri Tanzania ya viwanda.

Share This
Tags

Watanzania wametakiwa kupunguza unywaji wa pombe ili kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa kati kupitia viwanda kama inavyoelekezwa na serikali.

Hayo yamesemwa na Profesa Ayoub Maghimba Mkurugenzi msaidizi Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto leo Jijini Dar es Salaam.

Prof. Maghimba amesema kuwa unywaji wa pombe kupitiliza unasababisha magonjwa na kumfanya mtu ashindwe kushiriki katika shughuli yoyote ya Kimaendeleo.

“Pombe inasababisha saratani, uharibifu wa figo na magonjwa mengine lukuki kwaiyo ni vema watanzania wakatumia kiwango kidogo cha pombe ili kuepukana na hayo madhara yanayoweza kujitokeza.’’

Aidha Prof Maghimba akaeleza kiwango halisi cha pombe kinachopaswa kunywewa kwa mwanaume na mwanamke.

“mtumiaji wa kilevi hususani bia  ananatakiwa kunywa chupa mbili za bia kwa muda wa masaa mawili mwanamke anatakiwa kunywa chupa moja ya bia kwa muda wa masaa mawili pia wine mwanaume anatakiwa anywe glass mbili za wine kwa muda wa masaa mawili.’’

Naye Mratibu wa Magonjwa yasiyo ambukiza Bw. Shadrack Buswelu akaeleza matumizi mazuri ya unywaji wa pombe.

“matumizi mazuri ya pombe ni yale matumizi yanayohimil kile kiwango cha pombe mwilini cha 0.005.mwanaume anatakiwa kunywa chupa mbili na mwanamke kunywa chupa moja hii ni kutokana na mwanaume kuwa na enzim nyingi zaidi kuliko mwanamke.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>