Published On: Thu, Jan 19th, 2017

WINGI WA MIFUGO WACHANGIA UKAME KAGERA.

Share This
Tags

Wingi wa mifugo ambao hauendani ni maeneo ya malisho katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera umesababisha ngombe zaidi ya elfu nne kufa kutokana na kukosa malisho pamoja na maji baada ya ukame kuyakabili baadhi ya maeneo ya mkoa huo.

Betsela Byenobi  ni afisa mifugo wilaya ya Karagwe anasema kuwa  wingi wa mifugo katika wilaya hiyo hauendani na maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya malishohali hali iliyosababisha mifugo mingi kufa  baada ya ukame kuyakumba maeneo ya wilaya hiyo

Aidha afisa mifugo huyo amesema kuwa wingi wa mifugo ambao hauendani na maeneo yaliyopangwa unasababisha adhari kimazingira na kueleza kuwa tayali halimashauri imeisha tunga sheria ndogo zitakazosaidia kuondokana na ufugaji usio na tija

Asikofu mkuu wa dayosisi ya Karagwe wa kanisa la kiinjili kirutheri Tanzania (KKKT) Benson Bagonza na kusema ili mfugaji aweze kunufaika na mazao yatokanayo na mifugo,serikali ihakikishe inatenga maeneo ya kulisha mifugo na kuweka viwanda vya kusindika nyama na maziwa.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>