Published On: Wed, Jan 18th, 2017

SERIKALI YAPANIA KUBORESHA SEKTA YA AFYA.

Share This
Tags

Katika kuboresha huduma ya Afya nchini Serikali imetenga Shilingi Bilioni 251 huku mkoa wa Katavi ukipewa Shilingi bilioni 1.5 kuwezesha wakazi wa Mkoa wa huo kupata huduma bora ya afya.

Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa wakati akizindua duka la madawa la MSD katika Ziara yake ya Siku Moja Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi lililogharimu Shilingi milioni 55.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa MSD Raurean Lugambwa, ameleeza Duka hilo litakavyosaidia upatikanaji wa dawa na Tiba kwa Wakazi wa mkoa huo na mikoa jirani ya Tabora, Rukwa na Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Mhuga, amewahakikishia wakazi wa Mkoa huo kuanza kwa Ujenzi wa Hospitali yao kwa Mwaka huu wa fedha.

Mwaka huu wa Fedha Serikali imekusudia kusaidia wananchi kupata huduma bora ya afya ikilinganishwa na Bajeti iliyopita ya Shilingi Bilioni 29.2. pekee Nchi nzima

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>