Published On: Mon, Jan 16th, 2017

KUKU NCHINI MAREKANI WALETA MADHARA KWA PAKA.

Share This
Tags

Mamia ya Paka nchini Marekani wamelazimika kuwekwa Karantini baada ya kuambukizwa na maradhi ya Homa ya Kuku .

Kesi za maradhi hayo yanayoambukiza katika makaazi ya wanyama ya shirika moja la kuokoa wanyama zimeripotiwa katika wanyama kadhaa eneo hilo .

Idara ya afya ya New York ilifahmisha kuwa wanyama wengi pia wanaofugwa nyumbani pia wanaweza kuambukizwa maradhi hayo yanayosababishwa na virusi aina ya H7N2.

Kuna takriban wanyama 500 katika makaazi hayo na kati ya paka 386 walipatikana na ugonjwa huo .

Mwezi Novemba mwaka jana ilani ya maradhi hayo ilitangazwa baada ya paka kupatikana na ugonjwa huo katika makaazi ya wanyama yliyopo Manhattan .

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>