Published On: Mon, Jan 4th, 2016

WAZIRI MWIGULU AAGIZA KUVUNJWA KWA BODI YA NARCO KUTOKANA NA UFISADI.

Share This
Tags

Serikali imeagiza kuvunjwa kwa bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), inayosimamia ujenzi wa Machinjio ya kisasa, Ruvu chini Mkoani Pwani kwa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo.

Unapofika katika eneo hili la Ruvu chini na kushuhudia Ujenzi wa jengo hili la machinjio ya kisasa utabaini kuwa ujenzi wake umesimama kwa kipindi kirefu.

Kumbe nyuma ya pazia kuna jambo, linalomlazimu Waziri wa kilimo mifugo na Uvuvi, MWIGULU NCHEMBA kuingilia kati na kuvunja bodi inayosimamia ujenzi huo.

Kabla ya kuvunjwa kwa Bodi hiyo Waziri wa Kilimo, mifugo na uvuvi MWIGULU NCHEMBA amehoji masuali kadhaa kwa Kaimu Mkurugenzi wa NARCO, BWIRE KAFUMU baada ya kubaini matumizi mabaya ya fedha iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi huo.

Majibu ya watendaji wa NARCO yanamfanya Waziri kuagiza kuzuiliwa kwa malipo ya Mshauri wa ujenzi wa machinjio hiyo ya kisasa, na kuvunjwa kwa bodi iliyosimamia ujenzi huo.

Baada ya kukamilisha ziara katika jengo hilo Waziri akaagiza uchunguzi wa kina ufanyike dhidi ya wale waliohusika katika ubadhirifu huo.

Hadi kukamilika kwa ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa zaidi ya shilingi bilioni 10 zilipangwa kutumika huku Serikali ikiwa tayari imetoa zaidi ya bilioni tano ambazo zimezua sintofahamu hiyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>