Published On: Mon, Jan 4th, 2016

WATENDAJI TABORA WASHAURIWA KUWASAIDIA WAHITIMU WA JKT

Share This
Tags

Katika kuhakikisha vipaji vinaendelezwa na kuwaepusha vijana kujiingiza katika vitendo viovu, watendaji wa Halmashauri mkoani tabora wameshauriwa kuwaongoza vijana wanaomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa,JKT, kwa kuwapatia Ardhi, ikiwemo kuwashirikisha katika vikundi ili wafanye shughuli za uzalishaji mali.

Luteni Kanali AHMED ABAS AHMED ni mkuu wa kambi ya jeshi Msangi Tabora amebainisha hayo wakati wa kumaliza mafunzo ya miezi mitatu yaliyofanyika kambini hapo.

Kwa upande wake,LUTENI KANALI MANG’WEO,kwa niaba ya Mkuu wa JKT, anasema madhumuni ya jeshi hilo ni kuwajengea uwezo vijana hao.

Akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo,Mkuu wa Wialaya ya Tabora, SULEIMAN KUMCHAYA ,ameutaka uongozi wa kambi hiyo kuwapelekea viongozi majina ya vijana wanaohitimu ili waweze kuwasaidia.

Kwa upande wao wahitimu hao nao wakazungumzia ni kwa namna gani wameweza kunufaika kupitia mafunzo hayo.

Jumla ya wahitimu 642 wamehitimu mafunzo hayo katika kambi hiyo ya JKT Msange yaliyochukua miezi mitatu.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>