Published On: Thu, Jan 21st, 2016

REAL MADRID YAONGOZA KIMAPATO

Share This
Tags

Klabu ya Real Madrid imekuwa namba moja kwa kuingiza mapato kwa mwaka wa 11 mfululizo kwa mujibu wa Deloitte.

Klabu hiyo ilipata euro 577m (£439m) msimu wa 2014-15.

Mabingwa wa Klabu Bingwa Ulaya Barcelona wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na euro 560.8m (£426.6m), huku United wakiwa nambari tatu kwa kujipatia euro 519.5m (£395.2m).

Lakini Deloitte wamesema kuna uwezekano mkubwa sana kwamba United huenda ikawa nafasi ya kwanza kwa miezi 12 ijayo.

Manchester United walishuka kutoka nambari mbili hadi nambari tatu baada ya kushuka kwa mapato yao.

Kutokana na mkataba mpya wa haki za utangazaji katika runinga wa thamani ya £5.1bn utakaoanza msimu wa 2016-17, Real Mdrid huenda ikashuka kimapato.

Ligi ya Premia inaongoza kwa kuwa na klabu nyingi kwenye orodha ya klabu 30 tajiri, ikiwa na klabu 17,Hii inatokana na mikataba mizuri ya utangazaji na upeperushaji wa mechi.

West Ham wamefika kwenye 20 bora kwa mara ya kwanza tangu 2005-06, baada ya kupata mapato ya euro 160.9m (£122.4m).

Manchester United waliongoza orodha hiyo, ambayo kwa Kiingereza hujulikana kama Deloitte Football Money League, ilipozinduliwa mwaka 1998, walipoandikisha mapato ya jumla ya £87.9m.

ORODHA YA VILABU KIMAPATO DUNIANI

1 (1)    Real Madrid 577 (549.5)    439 (459.5)

2 (4)    FC Barcelona           560.8 (484.8)             426.6 (405.4)

3 (2)    Manchester United 519.5 (518)    395.2 (433.2)

4 (5)    Paris Saint-Germain            480.8 (471.3)             365.8 (394.1)

5 (3)    Bayern Munich        474 (487.5)    360.6 (407.7)

6 (6)    Manchester City       463.5 (416.5)             352.6 (348.3)

7 (8)    Arsenal          435.5 (359.3)             331.3 (300.5)

8 (7)    Chelsea         420 (387.9)    319.5 (324.4)

9 (9)    Liverpool        391.8 (305.9)             298.1 (255.8)

10 (10)  Juventus       323.9 (279)    246.4 (233.3)

11 (11)   Borussia Dortmund             280.6 (261.5)             213.5 (218.7)

12 (13)   Tottenham Hotspur 257.5 (215.5)             195.9 (180.2)

13 (14)    Schalke 04    219.7 (214)    167.1 (179)

14 (12)    AC Milan       199.1 (249.7)             151.5 (208.8)

15 (15)    Atletico de Madrid    187.1 (169.9)             142.3 (142.1)

16 (New)        AS Roma       180.4 (127.4)             137.2 (106.5)

17 (19)            Newcastle United    169.3 (155.1)             128.8 (129.7)

18 (20)            Everton          165.1 (144.1)             125.6 (120.5)

19 (17)            Internazionale          164.8 (162.8)             125.4 (136.1)

20 (New)     West Ham United     160.9 (139.3)             122.4 (116.5)

 

 

 

 

 

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>