Published On: Thu, Jan 21st, 2016

NYWILA ZILIZOTUMIWA SANA NA WATU 2015

Share This
Tags

Kampuni ya usalama mtandaoni ya SplashData imetoa orodha ya nywila au maneno ya siri yaliyotumiwa sana na watu mwaka uliopita.

Orodha hiyo imetayarishwa kwa kutumia maneno ya siri zaidi ya milioni mbili yaliyofichuliwa na wadukuzi mwaka uliopita.

Mwaka huu, neno ‘Star Wars’, kutoka kwa mwendelezo wa filamu za Star Wars, lilikuwa miongoni mwa maneno 25 yaliyotumiwa zaidi. Filamu ya Star Wars: The Force Awakens ilizinduliwa mwezi Desemba.

Wengi bado wanatumia ‘123456’ kama nywila na wengine ‘password’.

Ili kuwa salama mtandaoni, huwa ni vyema kutumia nyila ambayo watu wengine hawawezi wakaifikiria au kugundua kwa urahisi.

Moja ya njia za kuimarisha neno la siri ni kuchanganya tarakimu, herufi na alama pamoja na kuchanganya herufi kubwa na ndogo.

Lakini wengi hutatizika katika kukumbuka nywila.

Moja ya njia unazoweza kutumia ni kuangalia maneno ya wimbo uupendao na kuyafupisha.

Hapa, tunakupa mfano wa jinsi unaweza kupata nyila kutoka kwa wimbo.

  1. Chagua mwanamuziki umpendaye, tuseme kwa mfano Diamond Platinumz.
  2. Chagua wimbo, kwa mfano Mdogo mdogo
  3. Tafuta mstari mmoja, sana ukupendezao zaidi, mfano mstari wa kwanza: ‘Nimetembea tembea bara na visiwani’
  4. Fupisha kwa kuchukua herufi ya kwanza ya kila neon, au herufi mbili za kwanza. Tukichukua herufi mbili za kwanza, tunapata ‘Nitebanavi’
  5. Changanya herufi kubwa na ndogo, unaweza kupata kwa mfano ‘NiteBANAvi’ kutoka kwa mstari wetu.
  6. Kisha, badilisha herufi zinazokaribiana na tarakimu kuwa tarakimu, mfano badala ya ‘a’ tumia ‘@’ na badala ya ‘i’ tumia ‘1’.

Katika mfano wetu, tutapata ‘N1teB@N@v1’. Ni vigumu mtu kuigundua kwa urahisi lakini kila ukikumbuka wimbo wako unaweza ukaikumbuka kwa urahisi.

Nywila zilizotumiwa sana 2015

1. 123456

2. password

3. 12345678

4. qwerty

5. 12345

6. 123456789

7. football

8. 1234

9. 1234567

10. baseball

11. welcome

12. 1234567890

13. abc123

14. 111111

15. 1qaz2wsx

16. dragon

17. master

18. monkey

19. letmein

20. login

21. princess

22. qwertyuiop

23. solo

24. passw0rd

25. starwars

CHANZO: BBC Swahili

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>