Published On: Fri, Jan 22nd, 2016

MZEE YUSUF KUIPELEKA TAARABU KIMATAIFA.

Share This
Tags

IMG-20151229-WA0008

Mkali wa muziki wa taarabu ukanda wa Afrika Mashariki Mzee Yusuf ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo mpenzi Chocolate amebainisha mpango wake wa kuupeleka muziki huo wa mwambao kwenye soko la kimataifa.
Akizungumza na Shadee wa Clouds E ya Clouds TV, Mzee Yusuf amesema licha ya kufanya video kali hapa bongo amepanga kufanya video kali huko South Afrika ili kupata video bora itakayomtangaza kimataifa.
“Nimefanya video ya mpenzi chocolate hapa Tanzania, nimetumia helkopta na kila aina ya vifaa lakini still haikufanya vizuri, sasa nimepanga kuwafata maproduza wazuri ambao kazi zao zinapata airtime kwenye channel mbalimbali za kimataifa,” alisema Yusuf.
Katika hatua nyingine Yusuf amefagilia uamuzi wa CLOUDS TV kuingia kwenye king’amuzi cha DSTV kwa madai kwamba kazi zake zitakazorushwa huko zitaonekana kwenye nchi zaidi ya tisa duniani.
“Kwa sasa sizubiri tena foleni ya M-net, nimetumia fedha nyingi kuhakikisha nafanya video bora, ikipigwa ya Beyonce au Akon hakuna tofauti,” alisema mkali huyo wa Modern Taraab.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>