Published On: Mon, Jan 4th, 2016

MSAIDIZI WA IGP, MKE, WATOTO NA MSICHANA WA KAZI WAFA KWA MAFURIKO.

Share This
Tags
WATU wanane wamefariki dunia akiwemo mpambe wa (ADC), wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP, Inspekta Gerald. Ryoba kutokana na mafuriko ya mvua huko Kibaigwa mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, David Misiime, Mpambe wa IGP, akiwa na familia yake walikutwa na umauti baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam, kwenye barabara kuu ya Dodoma-Morogoro kusombwa na mafuriko ya maji yaliyokuwa yakienda kasi usiku wa kuamkia leo Januari 4, 2016 eneo la bwawani.
Akifafanua zaidi, Kamanda huyo wa polisi amewaambia waandishi wa habari mkoani Dodoma leo Januari 4, 2016 kuwa katika gari hilo kulikuwa na watu 6 ambao wote walifariki dunia na miili yao tayari imepatikana wakiwemo watu wengine wawili wakazi wa eneo hilo.
Kamanda Misiime amewataja marehemu kuwa ni pamoja na Gerald Ryoba ambaye ni msaidizi wa Mkuu wa jeshi la Polisi nchini, watoto ambao ni Gabriel Gerald Ryoba, Godwin Gerald Ryoba na mkewe Fidea John Kiondo.
Wengine ni Dereva wa gari hilo F.3243 Koplo Ramadhan, Msichana wa kazi aliyefahamika kwa jina la Sara mwenyeji wa mbinga Mkoani Ruvuma.

Wimbo wa kwaya ya Ambassadors of Christ ambao unaoimbwa kwa hisia kuu unawakumbusha wote walio hai kushukuru kujiuliza kwa nini upo hai hadi leo.

Na hivyo ndivyo ilivyo kwa kwa ndugu na jamaa wa familia ya Msaidizi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP ERNEST MANGU, Afande GERALD RIYOBA ambaye amefariki kwa kusombwa na mafuriko hawajuti tena na kilichobaki ni kumshukuru Mungu kwa upendo wake mkuu dhidi ya mpendwa wao huyo.

Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi aamin.., lakini msikose kujiuliza unajua makusudi ya mungu kukuacha hai mpaha leo?

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>