Published On: Fri, Jan 15th, 2016

MASHINDANO YA CHAN KUANZA KUTIMUA VUMBI KESHO

Share This
Tags

Michuano ya nne ya kombe la chan kwa 2016 itaanza kutimua vumbi kesho huko nchini Rwanda.

Michuano hii ya Chan inashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani tu, huku mataifa kumi na sita yakichuana kuwania ubingwa huo wa Afrika.

Wenyeji Rwanda wako kundi A wakiwa na mataifa ya Gabon, Morocco, Ivory Coast watatumia viwanja vya Amahoro na Stade Huye.

Kundi B lina timu za DR Congo, Angola, Cameroon na Ethiopia timu hizi pia zitatumia viwanja vya Amahoro na ule wa Stade Huye.

Katika kundi C kuna timu za Tunisia , Nigeria, Niger na Guinea timu hizi zitachuana katika viwanja vya Regional Nyamirambo na ule wa Umuganda.

Mataifa ya Zimbabwe Mali Uganda pamoja na Zambia wao wako kundi D, timu hizi zitatumia viwanja vya Umuganda na Regional.

Michuano hii itafikia tamati Februari 7 kwa mchezo wa fainali itakaopigwa kwenye dimba la Amahoro Jijini Kigali.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>