Published On: Thu, Jan 21st, 2016

MAPIGO YA MOYO YANAYOBADILIKA HATARI KWA WANAWAKE

Share This
Tags

Mabadiliko ya mapigo ya moyo ni ya hatari kwa wanawake zaidi kuliko wanaume, kwa mujibu wa tafiti 30 , zilizohusisha zaidi ya wagonjwa milioni nne.

Kwa mujibu wa utafiti huo wanawake wenye mapigo ya moyo yanayobadilika badilika (AF) walikuwa na uwezekano wa kufa kwa maradhi ya moyo ama kiharusi mara mbili zaidi.

Wanawake mara nyingi hawaponi vizuri kwa dawa za kudhibiti mabadiliko ya mapigo ya moyo ama hupatikana na maradhi ya moyo baadae kuliko wanaume.

“Uwezekano mmoja ni kwamba wanawake wenye mapigo ya moyo yanayobadilika hawatibiwi ipasavyo ikilinganishwa na wanaume ,” Connor Emdin na wenzake ,katika chuo kikuu cha Oxford, walieleza.

Wakati huo huo, wataalam wanasema madaktari hawanabudi kuelewa kuhusu uchunguzi huu ili kuepuka vifo vinavyoweza kuzuiwa.

Takriban watu milioni moja nchini Uingereza wana mapigo ya moyo yanayobadilika.

Unaweza kujichunguza mwenyewe ikiwa una tatizo hilo kwa kuhisi mapigo yako kwa sekunda 30.

Ni jambo la kawaida kuhisi mabadiliko ya mapigo ya moyo mara chache , mfano kukosa kwa pigo moja, kukosa kwa pigo moja ama mapigo zaidi, ni jambo la kawaida si jambo la kukutia hofu .

Lakini ikiwa ikiwa utahisi mapigo ya moyo yatabadilika kwa kipindi kirefu , unapaswa kumuona daktari.

Mapigo pia yanaweza kuwa ya kasi sana , zaidi ya mapigo 100 kwa dakika unapokua umetulia husababisha uchovu na kupungua kwa pumzi.

Dawa zinaweza kudhibiti hali hii na kuzuia hatari ya kiharusi (kuganda kwa damu ama kuvuja kwa damu kwenye ubongo).

CHANZO: BBC Swahili

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>