Published On: Mon, Jan 4th, 2016

MAMALISHE MWANZA WAOMBA KUFUTWA KWA AGIZO LA KUFUGWA KWA BISHARA

Share This
Tags

Baadhi ya wafanyabiashara wa chakula maarufu kama mama lishe jijini Mwanza, wameiomba serikali  ya awamu ya tano kufuta agizo la kufunga sehemu zao za biashara, kufuatia mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu kwa wale watakaokua wamekidhi vigezo vya usafi, kwakua linaathiri kipato chao na kushindwa kutimiza majukumu yao ya kila siku.

Siku chache zilizopita serikali ilipiga marufuku uuzaji wa vyakula mitaani ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Kipindupindu, agizo linaloendelea kutiliwa mkazo na viongozi jiji la Mwanza katika mapambano ya ugonjwa huo uliodumu takribani miezi sita sasa na kupoteza maisha ya baadhi ya watu.

Clouds TV imefanikiwa kufika katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza na kuzungumza na baadhi ya Mama Lishe nao walikua na ombi kufuatia agizo la serikali.

Takribani watu 25 wamepoteza maisha Mkoani Mwanza kutokana na ugonjwa wa kipindupind tangu ulipozuka  mwezi septemba mwaka jana na kusambaa katika Wilaya zote saba za Mkoa huu.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>