Published On: Thu, Jan 14th, 2016

LIBERIA NI MOJA YA NCHI AMBAZO HAZIKUTAWALIWA NA NCHI ZA ULAYA

Share This
Tags

Na Austin Beyadi,

Nchi ya Liberia ni moja ya nchi chache za kiafrika ambazo hazijatawaliwa na watu wa Ulaya, Badala yake, nchi hii ya Liberia ilikuwa ni makao ya watumwa waliorudishwa kutoka nchini Marekani baada ya kusitishwa biashara ya watumwa.

Nchi hii ndio nchi pekee ya kiafrika ambayo imeongozwa na raia wa kigeni kwa kipindi cha zaidi ya miaka mia moja huku rais wa kwanza mwenye asilia ya Liberia alipatikana mwaka 1980 baada ya mapinduzi yaliyomuondoa rais wa wakati huo.

Raia hao weusi wa Marekani walianzisha harakati za ukombozi mwanzoni mwa karne ya 19 kwa lengo la kujiondoa utumwani na kuunda nchi yao.

Kwa sababu hiyo kundi la Wamarekani weusi wenye asili ya Afrika lilihamia Magharibi mwa Afrika na kuasisi nchi ya Liberia kwa kusaidiwa na taasisi ya wahamiaji, baada ya kuwa utumwani kwa miaka mingi huko Marekani.

Awali Liberia ilikuwa ikiendeshwa kama moja ya majimbo ya Marekani, lakini mwaka 1847 nchi hiyo iliasisi mfumo wa jamhuri na rais wake wa kwanza akawa Joseph Roberts, mtumwa kutoka jimbo la Virginia.

Watumwa hawa ndiyo wakatumia kisomo chao kisha wakaanzisha serikali ambayo kwa kila namna inafanana na ile ya Marekani.

Neno “Liberia” linamaanisha “nchi ya watu huru.” Mwanzoni nchi hii ilipokaliwa na Wareno iliitwa Pwani ya Nafaka/Punje. Mji mkuu wa Liberia ulipewa jina lake, Monrovia, kutokana na jina la aliyekuwa rais wa Marekani na rais wa chama kilichokuwa kikiendesha kampeni ya kuhamisha waafrika weusi wa Marekani waliokuwa wameachiwa toka katika makucha ya utumwa

Rais huyo aliitwa James Monroe na chama hicho kiliitwa America Colonization Society.

Idadi ya wahamiaji wa kwanza, waliojulikana kama Americo-Americans, ilikuwa ni 86. Toka mwaka 1847 hadi 1861, watumwa walioachiwa huru waliohamia Liberia walikua 13,000.

Jeshi la majini la Marekani liliongoza juhudi za mikataba ya uhusiano mwema kati ya wahamiaji na wenyeji. Watu wengi hudhani kuwa Waafrika Weusi toka Marekani walipohamia nchi hiyo, hakukuwa na watu.

Kulikuwa na wahamiaji waliotoka sehemu mbalimbali kama Mali, Ghana, Sudan, n.k. Wahamiaji walijitofautisha na wenyeji kwa kutumia neno “Mr” kwa wanaume, na walishika sehemu zote muhimu za uongozi.

Rais wa kwanza wa nchi hiyo, Joseph Jenkins Roberts alizaliwa nchini Marekani. Rais wa kwanza mwenyeji toka makabila ya wenyeji (ambao hawakuhamia toka Marekani) alikuwa ni Sajenti Meja Samuel Doe aliyechukua madaraka kwa nguvu mwaka 1980.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>