Published On: Tue, Jan 19th, 2016

KONTA AMBWAGA VENUS WILLIAMS KATIKA TENISI

Share This
Tags

Mchezaji nyota wa tenisi kutoka Uingereza JOHANNA KONTA amemshinda VENUS WILLIAMS 6-4 6-2 na kufika raundi ya pili ya shindano la tenisi la Australian Open mjini Melbourne.

KONTA, 24, alipata ushindi kwa kutumia dakika 79 huku bingwa wa Grand Slam Williams, ambaye alikuwa amefungwa bendeji paja lake la kushoto, akionekana kutatizika.

KONTA, aliyefika hatua ya 16 bora katika US Open mwaka 2015, sasa atakutana na mshindi kati ya CARINA WITTHOEFT na SAISAI ZHENG, katika raundi ya pili.

KONTA aliyeorodheshwa nambari 47 duniani, alikuwa akicheza mara ya kwanza katika Australian Open na ndiye mwanamke Mwingereza pekee aliyesalia katika droo ya mashindano ya mchezaji mmoja mmoja baada ya HEATHER WATSON kushindwa Jumatatu.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>