Published On: Thu, Jan 21st, 2016

JE, WAJUA KUHUSU MTO AMAZON?

Share This
Tags

Na Austin Beyad

Mto Amazon ni mto mkubwa duniani. una chanzo chake katika milima ya Andes inavuka beseni yake hadi Atlantiki kupitia eneo kubwa la misitu minene.

Sehemu kubwa ya mwendo wake iko katika nchi ya Brazil. Unabeba maji zaidi kuliko mito ya Nile, Mississippi na Yangtse pamoja

Mto huu  unapatikana Amerika ya Kusini, ni mkubwa kuliko mito yote duniani na hatari sanaa kwasababu ya urefu wake na upana wake.

Kwakuwa mto huo ni mkubwa kuliko mito yote duniani ulipewa jina jingine ambalo ni “River Sea” likiwa na maana ya  “Mto bahari”.

Mto huu una kina zaidi ya futi 50 na ni mkubwa kiasi cha kutokuwa na uwezo wa kupatikana sehemu za kuungia daraja kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Kuhusu urefu hakuna mapatano bado kama Nile au Amazonas ni mto mrefu duniani. Makadirio hutegemea ni tawimto upi mwenye chanzo cha mbali zaidi unaokubaliwa na wataalamu. 1969 urefu wake ulipimwa kuwa kilomita 6,400

Amazon ina tawimito zaidi ya 10,000 na kati ya hizi kuna 17 zenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,600 zikishinda mito kama Senegal, Gambia au Nile ya buluu.

Upana wa mto ni wa kilomita kadhaa kufika hadi kilomita 100 wakati wa mafuriko ya kila mwaka.

Delta ya Amazonas ina upana wa mamia ya kilomita; ndani yake kuna kisiwa cha Marajó chenye eneo la kilomita za mraba 49,000 ambalo ni kubwa kushinda nchi kama Rwanda au Burundi.

Amazonas ni njia muhimu ya mawasiliano na usafiri nchini Brazil.

Meli kubwa za baharini zinaweza kuingia hadi bandari ya Manaus iliyoko kilomita 800 ndani ya bara.

Meli ndogo za baharini hadi uzito wa tani 3,000 zinaweza kuvuka Brazil yote na kufika Peru.

Mto huo huanza ukiwa kijito katika Milima ya Andes ya Peru yapata kilometa 160 kutoka kwenye Bahari ya Pasifiki, kisha huungana na mito mingine na kushuka kwa mteremko wa meta 5,000 hivi hadi Bahari ya Atlantiki.

Mto huo huitwa majina tofauti kabla haujaingia Brazili, ambako kwanza unaitwa Solimões.

Karibu na Manaus, mto huo huungana na Mto Negro, ambao ndio mto mkubwa zaidi unaoingia humo, na hapo ndipo unapokuwa mto mkubwa wa Amazon.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>