Published On: Wed, Jan 6th, 2016

GUARDIOLA AMSHAURI MESSI KUHAMIA LIGI KUU ENGLAND.

Share This
Tags

Kocha wa Leicester city Claudio Ranieri ametuma ofa ya pauni milioni mbili kwaajili ya kumsajili kiungo Nigel De Jong, kutoka Ac Milan , wakati huo huo Leicester city inataka kumsajili mshambuliaji wa Porto Vincent Aboubakar ili ampe changamoto Jamie Vardy.

Vilabu vya Arsenal na Liverpool vinagombea saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang .

Kuna taarifa zinazodai kocha Pep Guardiola anafanya mazungumzo na wawakilishi wa manchester City na United, baada ya kukataa ofa ya Chelsea, Milan na Paris Saint-Germain. Pep anamshawishi mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ajiunge nae kwenye ligi kuu ya England.

Klabu ya Real Madrid na Chelsea huenda zikabadilisha wachezaji Gareth Bale kwenda Chelsea huku Eden Hazard akijiunga na Real Madrid.

Timu za Crystal Palace na Watford zinafanya mazungumzo na Emmanuel Adebayor ambaye hana timu kwa sasa.

Watford ipo karibu kabisa kumnasa Mario Suarez.
Kamati ya maadili ya FIFA imependekeza katibu mkuu wa shirikisho hilo linalosimamia soka duniani Bw Jerome Valcke afungiwe miaka tisa.

Anadaiwa kutumia vibaya pesa pamoja na kukiuka sheria nyingine za Fifa.
Kamati hiyo imependekeza Valcke azuiwe kushiriki shughuli zozote za michezo kwa siku nyingine 45, juu ya marufuku ya siku 90 ambayo ameitumikia, kusubiri uamuzi kuhusu kufungiwa ya miaka tisa waliyoipendekeza.

Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya nchini Marekani Kobe Bryant atakosekana katika mchezo wa alfajiri ya kesho dhidi ya Golden State Warriors kutokana na maumivu ya bega.

Kauli juu ya kuumia kwa Kobe imetolewa na kocha wa Lakers Byron Scott ikiwa ni muda mchache kuelekea katika mchezo huo.Huu utakuwa mchezo wa tatu kwa Kobe kuukosa tangu acheze mchezo dhidi ya Boston Desemba 30.
Kuna uwezekano wa Kobe kurejea katika mchezo dhidi ya Sacramento Kings siku ya Alhamisi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>