Published On: Mon, Jan 4th, 2016

AJALI YAUWA WANNE IRINGA

Share This
Tags

Tuanzie huko mkoani iringa ambapo Watu wanne wamefariki dunia na wengine 37 wamejeruhiwa kufuatia ajali iliohusisha basi la kampuni ya LUWINZO, lenye namba za usajili T782 AZR inayofanya safari zake kutoka Njombe kwenda Dar es salam na Loli lenye namba za usajili T718 CRV IVECO lililokuwa likitokea songea kwenda dar es salam ambalo ilikuwa inajaribu kulipita gari jingine na kuligonga lori hilo kwa nyuma.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoani Iringa PETER KAKAMBA, amesema ajali hiyo imetokea eneo la MBALAMAZIWA nje kidogo ya mji wa mafinga.

Kamanda KAKAMBA amesema ajali hiyo imetokana na mwendokasi wa dereva wa basi hilo na imesababisha vifo vya watu 4 wawili miongoni mwao wametambuliwa kwa majina kuwa ni RASHID KIBADALE (47) ambaye ni kondakta wa basi na SALUM CHANGULA (28) ambaye ni Mkaguzi wa kampuni na kusababisha majeruhi 37 ambao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi.

Naye Mganga mfawidhi Hospitali ya wilaya Mufindi INOSENT MUHAGAMA, amekiri kupokea majeruhi 32 na mwili mmoja ambapo mmoja wa majeruhi alipoteza maisha nusu saa wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Taarifa zaidi tunaendelea kufuatilia na tutakujulisha.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>