Published On: Wed, Nov 11th, 2015

WATENDAJI BUKOBA WAWEKA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU.

Share This
Tags

Viongozi na watendaji mbalimbali katika manispaa ya Bukoba, wamefanya kikao na kupanga mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu ili usiingie na kuenea, katika manispaa hiyo, kufuatia taarifa za watu wenye dalili ya ugonjwa huo.

Akizungumza katika kikao kilichowashirikisha wenyeviti wa mitaa, watendaji wa  kata na watumishi wa idara ya afya, mganga mkuu wa wilaya  hiyo HAMZA MGULA, amesema kuwa hadi sasa, wagonjwa wawili wamelazwa katika kituo maalumu, kilichoandaliwa kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu eneo la Nshambya, na wanaendelea kuhudumiwa, na kwamba  wagonjwa waliowapokea wamefanyiwa vipimo na kugundua kuwa hawana ugonjwa huo.

Akizungumza katika kikao hicho mkuu wa wilaya ya Bukoba, JACKSON MSOME, amesema kwa mujibu wa taarifa za kitaalam bado ugonjwa wa kipindupindu haujaingia katika wilaya hiyo.

 Aidha viongozi hao wa mitaa walioshiriki katika kikao hicho wamesema kuwa elimu kwa wananchi inaitajika ili kuweza kuepukana visababishi vinavyoweza kueneza ugonjwa huo.

 Clouds TV ikaingia mitaani na kuzungunza na wananchi wanaofanya shughuli zao karibu na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kukusanyia takataka na haya ndio maoni yao.

 

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>