Published On: Fri, Nov 13th, 2015

WAKAZI WAISHIO PEMBEZONI MWA MTO MBEZI WAONYESHA HOFU YA MAFURIKO.

Share This
Tags

Wakazi waishio kando ya mto Mbezi maeneo ya Kawe Mji Mpya kata ya Kawe Mzimuni wameiomba serikali kuingilia kati ujenzi wa uzio katika mto Mbezi unaofanywa na kanisa ili kuwaepusha na mafuriko msimu wa mvua.

Clouds FM imefika katika mto huo na kushuhudia ujenzi huo ambao wakazi wa eneo hilo wamaeleza kuwa endapo ujenzi huo utaendelea ni dhahiri kuwa maisha yao yatakuwa hatarini pindi mvua zitakapoanza kunyesha.

Ni upi wito wa wananchi hao kwa mamlaka husika ili kuhakikisha wanakuwa salama pindi mvua zitakaponyesha?

Ili kubaini hatua za awali zilizoanza kuchukuliwa, Clouds fm imezungumza na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kawe Mzimuni ambapo anaeleza kuwa wameamua kusimamisha ujenzi huo. 

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>