Published On: Wed, Nov 11th, 2015

MGODI WA MADINI KUJENGWA WILAYANI ULANGA.

Share This
Tags

TANZANIA ni miongoni mwa nchi zenye madini  ya aina mbalimbali  kama ilivyo kwa nchi za Afrika na duniani kwa ujumla  na miongoni mwa madini hayo ni  madini ya kinywe (Graphite) ambayo hutumika kwa ajili ya kutengenezea bidhaa mbalimbali.

Barani Afrika ni nchi tatu tu ambazo zimebainika kuwepo kwa madini hayo ikiwemo Tanzania,Msumbiji na Mauritius  na kwamba hapa nchini madini hayo yamebainika kuwepo katika  mkoa wa Morogoro  wilayani  Ulanga,Ruvuma wilayani Songea,Tanga,Arusha na Lindi.

Katika wilaya ya Ulanga kampuni ya madini ya  KIBARAN inatarajia kujenga mgodi wa uchimbaji wa madini ya kinywe (Graphite) na kwamba kuwepo kwa mradi huo kunaweza kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa wananchi wa eneo hilo.

Katika kufanikisha mradi huo wa madini ya Kinywe  nini wito  kwa wadau mbalimbali ili mradi huo? Mkurugenzi huyo anabainisha..

 Naye mtaalam wa miamba  kutoka kampuni ya Tanzania Graphite, FREDERICK NGELEJA, amesema madini ya kinywe ya hapa nchini ni madini bora ikilinganishwa na madini kutoka nchi nyingine.

Nao waandishi wa habari wanatajwa kuwa na mchango mkubwa katika kuelimisha jamii kuhusiana na masuala mbalimbali ya uwekezaji hapa nchini.

Kampuni  ya  uchimbaji madini ya Kibaran inatarajia kutoa mafunzo kuhusiana na sheria ya madini ya mwaka elfu mbili na kumi na umuhimu wa uwekezaji katika sekta ya madini katika maeneo mbalimbali nchini kwa waandishi wa habari.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>