Published On: Wed, Nov 11th, 2015

MAHIZA ALIA NA KUKOSEKANA KWA HOSPITALI WILAYA YA MKINGA.

Share This
Tags

MKUU wa Mkoa wa Tanga MWANTUMU MAHIZA, amesema ni jambo la aibu kwa halimashauri ya Mkinga ambayo imeanzishwa miaka sita iliyopita, kukosa hospitali ya wilaya, ambapo kwa sasa halmashauri ya wilaya ya hiyo, inategemea vituo vya afya na hospitali ya rufani ya Bombo mkoani Tanga.

Katika ziara ya mkuu huyo wa Mkoa , MWANTUMU MAHIZA, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo AMINA KIWANUKA, akatolea ufafanuzi jambo hilo.

Hata hivyo mkuu wa Mkoa huo amehimiza mpaka ifikapo january 2016, hospitali hiyo iwe imeanza kujengwa kwa manufaa ya wananchi wa wilaya ya Mkinga.

Mahiza ambaye amehamishiwa mkoani tanga hivi karibuni, amesema hayuko tayari kuona watendaji wakishindwa kusimamia shughuli za maendeleo wakati wanalipwa mishahara kwa ajili hiyo.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>