Published On: Wed, Nov 11th, 2015

JESHI LA POLISI MTWARA YAKAMATA VIFAA VYA MLIPUKO.

Share This
Tags

JESHI la Polisi Mkoani Mtwara kwa kushirikiana na MARINE PARK,  pamoja na Kikosi maalum cha Taifa kinachoshughulikia uhifadhi wa mazingira pamoja na bahari, wamefanikiwa kukamata vifaa mbalimbali vya milipuko vinavyotumika katika uvuvi haramu katika bahari ya hindi. 

MWAIBAMBE, amesema wameanzisha operesheni maalum katika bahari ya hindi, ili kukabiliana na uvuvi haramu, ambapo katika operesheni hiyo wamefanikiwa kuwakamata watu watatu vinara wa mtandao huo.

 

Hata hivyo Kamanda MWAIBAMBE, ameomba wananchi mkoani humo kutoa ushirikiano ili kuwafichua watu hao ambao wanaharibu mazalia ya samaki na mazingira.

Aidha Kamanda MWAIBAMBE amesema Novemba 15 mwaka huu utafanyika uchaguzi wa mbunge katika jimbo la LULINDI, Mkoani Mtwara, baada ya kuahirishwa oktoba 25 mwaka huu kufuatia  kukosewa kwa majina ya baadhi ya wagombea,  na hivyo ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kurejea majumbani mara tu watakapomaliza kupiga kura na kutii sheria bila shurti.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>