Published On: Mon, Nov 9th, 2015

BAADHI YA WASOMI WATOA MATARAJIO YA SIFA ZA WAZIRI MKUU AJAE.

Share This
Tags

Baadhi ya wasomi na wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini wametoa maoni na mapendekezo yao kuhusu waziri mkuu ajae huku wakieleza kuwa wanatarajia kumpata waziri mkuu mchapakazi kama alivyo Raisi wa Tanzania DR.JOHN MAGUFULI.

Clouds Tv imezungumza na baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam akiwemo mhadhiri idara ya sayansi ya siasa na uongozi kutoka chuo kikuu huria cha Tanzania DR. LAZARO SWAI  ambapo anabainisha sifa wanazozitarajia kwa waziri mkuu atakaeteuliwa.

Tangu alipoapishwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania DR. MAGUFULI ameshafanya ziara za kushtukiza katika wizara ya fedha, hospitali ya taifa Muhimbili pamoja na kufanya mkutano na makatibu wakuu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi serikalini.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>