Published On: Fri, Nov 13th, 2015

ANNE MAKINDA ATOA MTAZAMO WAKE KUUSU SPIKA AJAE.

Share This
Tags

Vuguvugu kubwa limeigubika tasnia ya siasa katika kusaka nafasi ya Uspika wa Bunge ili kuliongoza Bunge la 11 ambapo wanasiasa lukuki wakiwemo wabunge wateule na wasiokuwa wabunge wamejitokeza kuwania nafasi hiyo.

Tangu kukamilika kwa zoezi la uchaguzi mkuu na kupatikana kwa wabunge, madiwani na Rais habari ya Mjini sasa ni Spika wa Bunge ambapo vigogo kadhaa wakiwemo wabunge wateule na wasiokuwa wabunge wamejitosa kwenye kinyang’anyiro hicho cha kutaka kuongoza Bunge la 11 huku Spika wa Bunge anayemaliza muda wake ANNE MAKINDA akimtaja anayetakiwa kuwa mrithi wake.

Spika huyo ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo mkubwa kwa muhimili wa Bunge nchini ametangaza kuachana na Uongozi wa kisiasa na kutaja mambo anayojivunia kuyafanya katika kipindi chake cha Uongozi.

Clouds Tv pia ikazungumza na wasomi mbalimbali ili kupata mitazamo yao kuhusu Spika ajaye akiwemo Dk. AYOUB RIOBA anayetaja namna Spika ajaye anavyotakiwa kuwa.

ANNE MAKINDA ni Spika wa Tatu kuendesha Bunge la vyama vingi, ambapo Spika wa kwanza alikuwa PIUS MSEKWA akafuatiwa na SAMWEL SITTA, ambapo mara Bunge la 11 litakapoanza kazi kubwa itakayotangulia ni kumtafuta Spika wa Bunge shughuli itakayoongozwa na Katibu wa Bunge Dk. THOMAS KASHILILA.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>