Published On: Wed, Nov 11th, 2015

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA MPYA KWA WATEJA WAKE.

Share This
Tags

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel imezindua ofa maalum itakayowawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa marafiki na familia bure ili kurahisisha ukuaji wa uchumi hasa kuelekea katika msimu huu wa mwisho wa mwaka.

Akizungumzia mpango huo Meneja Uhusiano wa Airtel  JACKSON MMBANDO amesema promosheni hiyo ijulikanayo kama OKOA MAPENE imelenga kuinua huduma za kifedha nchini huku ukiwapatia wateja njia rahisi ya kufanya miamala yao ya kila siku.

Kwa upande wake Meneja wa Airtel Money STEPHEN KIMEA amesema ofa ya OKOA MAPENE haitaathiri utendaji kazi wa mawakala wa Airtel Money kwani gawio lao litaendelea kuongezeka kama kawaida.

Hivi karibuni Airtel imewazawadia wateja wake kwa kuwapatia gawio la faida watumiaji wote wa huduma ya Airtel Money na kuwawekea moja kwa moja kwenye akaunti zao za simu.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>