Published On: Thu, Oct 15th, 2015

TACCEO YALALAMIKIA WALEMAVU KUBAGULIWA KATIKA MIKUTANO YA SIASA.

Share This
Tags

Mtandao wa asasi za kufuatilia chaguzi Tanzania TACCEO, chini ya kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC, wamebaini pia changamoto hiyo, kupitia taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa mtandao huo MARTINA KABISAMA, wakati akizungumzia mwenendo wa kampeni za uchaguzi.

Mwenyekiti huyo, ameeleza kuwa ni vyema wanasiasa wakatumia mikutano hii iliyobaki, kuweka watu watakaowasaidia watu wenye mahitaji maalumu kupata taarifa.

Nae mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu DR. HELEN KIJOBISIMBA, ameeleza kuwa zoezi la uandikishaji na uhakiki katika daftari la kudumu la wapiga kura, liligubikwa na changamoto nyingi zinazohitaji kupatiwa ufumbuzi.

Aidha ameeleza kuwa wanafunzi wengi wa vyuo, watakosa haki yao ya msingi ya kupiga kura, hivyo tume ya uchaguzi inatakiwa kuliangalia hili kwa jicho la tatu.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>