Published On: Thu, Oct 15th, 2015

MAMA REGINA LOWASA AWATAKA WATANZANIA KUCHAGUA VIONGOZI WATAKAO WASAIDIA

Share This
Tags

Watanzania wametakiwa kuwachagua viongozi wanaoweza kuwasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kutokana na sera wanazozitoa katika majukwaa ya kampeni.

Akizungumza na wakazi wa Jimbo la Iringa Mjini, Mke wa mgombea Urais kupitia chama cha Demorasia na Maendeleo CHADEMA kwa mwamvuli wa UKAWA mama REGINA LOWASA amesema, huu ndiyo wakati wa watanzania kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura, na kuwachagua viongozi wenye dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo, na wananchi kuwapigia kura viongozi wanaotokana na UKAWA.

Akinadi sera za chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema, mgombea Ubunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji PETER MSIGWA, amewaomba wananchi wa jimbo hilo kuendelea kumwamini ili akamilishe dhamira yake ya kuwaletea maendeleo, kwa kushirikiana na madiwani.

Akiwanadi wagombea Udiwani wenzake, mgombea Udiwani kata ya Mivinjeni FRANK NYARUSI ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA Iringa mjini, amewataka wananchi kuwachagua madiwani wanaotokana na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, ili waweze kubadilisha utendaji wa Halmashauri hiyo.

Katika hatua nyingine huko wilayani biharamulo mkoani Kagera, katika mkutano wa kunadi sera za chama cha CHADEMA, mgombea urais wa chama hicho EDWARD LOWASA, katika kumkumbuka hayati baba wa taifa mwalimu JULIUS NYERERE,

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>