Published On: Fri, Oct 30th, 2015

JOHN POMBE MAGUFULI RAIS MTEULE WA AWAMAU YA TANO TANZANIA

Share This
Tags

Hatimaye aliyekuwa mgombea urais wa chama cha mapinduzi CCM JOHN POMBE MAGUFULI, ametangazwa kuwa mshindi wa urais wa uchaguzi uliofanyika nchini Oktoba 25 mwaka huu.

JOHN MAGUFULI anakuwa rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akipata ushindi huo dhidi ya wagombea wenzake saba waliokuwa wakigombea nafasi hiyo.

Rais JOHN MAGUFULI aliyekabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, EDWARD LOWASA, amefanikiwa kupata kura milioni 8,882,935 sawa na asilimia 58.46, huku EDWARD LOWASA akipata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97.

Ushindi huo umetangazwa na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC DAMIAN LUBUVA katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu nyerere jijini Dar es salaam, mbele ya vyama sita vilivyosaini kukubaliana na matokeo kati ya nane.

Mwenyekiti huyo amebainisha utaratibu wa matokeo hayo kutangazwa kwa mujibu wa ibara ya 41 kifungu kidogo cha sita cha katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwa rais na makamu wake.

Kati ya wapiga kura milioni 23, 161, 440 walioandikishwa, waliopiga kura 15,589,639 sawa na asilimia 67.31, huku kura halali zikiwa ni 15, 193,862 sawa na asilimia 67.46, na kura zilizokataliwa ni 402,248 sawa na asilimia 2.58.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>