Published On: Fri, Oct 30th, 2015

CUF YATOA TAMKO

Share This
Tags

 Baada ya tamko la jana la  Jecha Salim Jecha ambae ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi wa Zanzibar , leo hii Chama cha wananchi (CUF) kimetoa hoja zao dhidi ya uamuzi huo.

Akizungumza na clouds fm makao makuu ya chama hicho Mtendeni Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad amefafanua hoja hizo ambazo walikaa pamoja na jopo la wanasheria kujadili zaidi suala la kufutwa uchaguzi.

Wakati huo huo kwa upande wa baadhi ya vyama vingine vya siasa huko Zanzibar, vikijumuisha chama cha Demokrasia Makini, SAU, CHAUMA, NRA, JAHAZI ASILIA na DP, vimekutana na waandishi wa habari na kutoa msimamo wao wa  kutokubaliana na tamko la mwenyekiti wa tume hiyo.

Aidha vyama hivyo vimeamua kulipeleka mahakamani shirika la utangazaji Zanzibar (ZBC ), na kumfungulia kesi mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar JECHA SALIM JECHA .

Jumla ya vyama 14 vilishiriki uchaguzi wa urais wa Zanzibar kwenye uchaguzi uliofutiwa matokeo jana.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>