Published On: Thu, Oct 15th, 2015

CHAVITA YALIA NA KUKOSEKANA KWA WAKALMANI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI.

Share This
Tags

Siku kumi kabla taifa halijashiriki kupiga kura kuwachagua madiwani, wabunge na rais, Chama cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) kimeilalamikia tume ya taifa ya uchaguzi kwa kutoa taarifa likuki za masuala ya uchaguzi, bila kuwepo kwa wakalimani wanaotafsiri maelekezo hayo.

Wakizungumza katika mafunzo kuhusu ushiriki wa viziwi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa usaidizi wa kutafsiriwa, mjumbe wa bodi ya CHAVITA  taifa SELINA LEMA amesema, kumekuwa na maelekezo ya msingi ambayo yamekuwa yakitolewa na tume hiyo, lakini kwenye mikutano ya tume na hata kwenye vyombo vya habari, hakuna wakalimani wa lugha ya alama, jambo linaloweza kuleta madhara kwa viziwi, iwapo watafanya kitu kinyume na maelekezo ya tume kwa kuwa elimu haijawafikia.

Nao makamu mwenyekiti wa CHAVITA taifa ODAVIA LUGAKINGIRA, na mratibu wa CHAVITA taifa BW.  STADIUS KONGOKA  wamesema, mafunzo hayo yatasaidia kuwapa elimu viziwi kuhusu taratibu za kuzingatia kwenye zoezi la upigaji kura, huku wakilishukuru shirika la Foundation For Civil Society kwa kuwasaidia kupata elimu hiyo, na kwamba wataipeleka kwa wenzao katika mikoa mbalimbali.

Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni wakili wa kujitegemea NOVATH RUKWAGO, ametolea ufafanuzi kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili viziwi, huku akiiomba tume kuangalia namna ya kusaidia makundi maalum, hususan viziwi katika kutoa maelekezo hayo.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama cha Viziwi Tanzania makao makuu, na  kushirikisha viongozi wa  CHAVITA kutoka mikoa mbalimbali nchini, kwa ufadhili wa shirika la The Foundation For Civil Society.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>