Published On: Tue, Jul 7th, 2015

WATANZANIA WASHAURIWA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA.

Share This
Tags

Na JAMES LYATUU

 

Katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii wa ndani,shirika la hifadhi za taifa TANAPA wameanzisha kampeni ya miezi sita yenye lengo la kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi za taifa ili kusaidia kukuza uchumi kupitia utalii.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salam na mkurugenzi wa utalii na masoko wa TANAPA IBRAHIM MUSSA wakati alipokuwa akizungumzia vivutio vinavyopatikana hapa nchini ambapo ameeleza kuwa huu ni wakati muafaka kwa wananchi kujijengea utaratibu wa kutembelea vivutio vya utalii.

Kwa upande wake kaimu meneja masoko wa TANAPA VICTOR RAFAEL ameeleza kuwa ili kuhamasisha wazawa kutembelea vivutio vya utalii shirika hilo limeweka tozo kidogo na kutoa zawadi mbalimbali kwa wananchi wanaokwenda kutembelea vivutio vya utalii.

Nae msemaji wa wizara ya maliasili na utalii DOREEN MAKAYA ameeleza kuwa vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika katika kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii.

Kwa mujibu wa TANAPA takwimu ya watanzania wanaokwenda kutembelea vivutio vya utalii kwa mwaka ni 450,000 na raia wa kigeni wakiwa ni 550,000 jambo linaloonyesha kuwa bado kuna mwamko mdogo kwa watanzania.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>