WAKAZI WA ITILIMA WALILIA HUDUMA ZA SIMU
Baadhi ya Wakazi wa wilaya ya itilima mkoani simiyu wameyaomba makampuni ya simu za mkononi kupeleka huduma za mawasiliano wilayani humo kutokana na kadhia ya kutafuta mawasiliano ambayo wanaipata kwa sasa.
Wakazi hao wa vijiji vya laini,mwaswale na lumwa,wamesema wanalazimika kupanda juu ya miti na wengine kwenye mapaa ya nyumba kwa ajili ya kupata mawasiliano jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao.