Published On: Wed, Jun 3rd, 2015

JAMII YASHAURIWA KUTUNZA NA KULINDA MAZINGIRA.

Share This
Tags

Katika kuadhimisha wiki ya mazingira Duniani, jamii imeshauriwa kulinda na kutunza mazingira hali itakayosaidia kufanya mazingira kuwa safi na kuondokana tatizo la magonjwa ya mlipuko.

Wito huo umetolewa jijini Dar es salam na Kamanda wa kikosi cha MMJKT, Luteni Kanali PETER MNYANI wakati jeshi hilo lilipokuwa likiendesha zoezi la ufanyaji usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wakazi wanaoishi kando ya mto Mlalakuwa ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya wiki ya mazingira Duniani.

Ameeleza kuwa kama kila mwananchi akiona ana jukumu la kulinda na kutunza mazingira itasaidia kufanya mazingira kuwa rafiki kwa kizazi cha sasa na kizazi cha baadae.

Kauli hiyo inaungwa mkono na mwakilishi wa taasisi ya Borda Tanzania inayojihusisha na masuala ya mazingira JACOB WOELK ambapo anatumia nafasi hiyo kuzitaka mamlaka zinazohusika na utunzaji wa mazingira kuwaelimisha wananchi kuhusiana na faida na athari za uharibifu wa mazingira.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>